Home EURO 2020 FODEN HATARINI KUIKOSA FAINALI EURO

FODEN HATARINI KUIKOSA FAINALI EURO


MSHAMBULIAJI kinda wa kikosi cha klabu ya Machester City na timu ya Taifa ya England, Phil Phoden yupo katika hatari ya kuukosa mchezo wa fainali ya michuano ya Euro 2020, kufuatia majeraha madogo aliyoyapata jana Ijumaa.

Kikosi cha England kimekamilisha maandalizi yao kuelekea mchezo huo wa fainali, katika mazoezi yaliyofanyika kwenye kituo cha mazoezi cha St George’s.

Kikosi hicho cha kocha Gareth Southgate kina nafasi ya kumaliza ukame wa muda mrerfu wa kushinda kombe katika michuano mikubwa wakicheza kwenye ardhi yao ya nyumbani, ambapo mara ya mwisho kufanya hivyo ni katika michuano ya kombe la dunia ya mwaka 1996.

Nyota wote 25 walikuwa sehemu ya mazoezi hayo ya mwisho ya England, huku Foden akiwa ndiye nyota pekee akliyepumzishwa. Uamuzi wa kumuondoa Foden katika mazoezi hayo ya mwisho ulifanywa na madaktari wa kikosi hicho juzi Ijumaa.

SOMA NA HII  HAALAND AMPA PONGEZI NYOTA ENGLAND

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here