Home Yanga SC ISHU YA MORRISON CAS BADO NZITO, MPILI ABAINISHA KUHUSU KIGOMA

ISHU YA MORRISON CAS BADO NZITO, MPILI ABAINISHA KUHUSU KIGOMA


HAJI Mpili, maarufu kama Mzee Mpili ambaye ni mwanachama wa Klab ya Yanga amesema kuwa laiti kama mchezaji Bernard Morrison angekuwa ndani Yanga angafanya vizuri zaidi tofauti na sasa.

Morrison amekuwa kwenye mvutano mkubwa na Yanga ishu ya mkataba wake ambapo Yanga wamekuwa wakidai kwamba ana dili la miaka miwili na mchezaji anadai kwamba dili lake lilikuwa ni la miezi sita lilikwisha.

Kuhusu hilo ambapo Yanga wameeleza kuwa kesi yake ipo kwenye ahakama ya usuluhishi, (Cas) Mzee Mpili amebainisha kuwa kesi hiyo ni nzito.

Mpili amesema:-“Akili yake waliivuruga na mimi naamini kama angekuwepo Yanga basi angefanya vizuri sana tofauti na sasa, kwa sababu wanasema hayupo kwenye timu ameondoka.

 


“Ndio maana tumepeleka CAS na kesi yake ni nzito na Morisson mwenyewe alitaka kesi yake iamuliwe hapa na mpira wake umeshapotea.


“Tarehe tatu alionyesha kama shoo tu hakufanya chochote kwani tulizuia mpira wake, na kwenye simu yangu sina namba ya Morisson na siwezi kuongea nae.

 

“Mzee Dalali amesema anatangulia kigoma na anaenda kunipiga lakini akumbuke kuwa na Haji Manara alisema hivo hivo kuwa atanipiga tatu kwenye mchezo uliopita na nilimpiga na hela katoa, sahizi sio bao moja itakuwa zaidi ya kuhesabu.

 

“Sisi hatuwezi kubadilisha uwanja ni ule ule pale pale kigoma sisi mipango ya kucheza mpira tumeshamaliza na watu wangu wameshafika.


“Simba wana kikosi kizuri lakini mimi na wachezaji wangu wa kuokota okota nitawapiga hivo,” .

SOMA NA HII  KISA SIMBA KUPIGWA JANA....YANGA WAIBUKA NA TAMKO LAO...INJINIA HERSI AJA NA HILI JIPYA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here