Home news ISHU YA MWAMUZI KOMBA KUINGIA UWANJANI SIMBA V YANGA IPO HIVI

ISHU YA MWAMUZI KOMBA KUINGIA UWANJANI SIMBA V YANGA IPO HIVI


 MWAMUZI mwenye beji ya FIFA, Frednand Chacha amesema kuwa kitendo cha mwamuzi msaidizi kwenye mchezo wa Simba dhidi ya Yanga, Frank Komba kuacha mstari na kuingia uwanjani alikuwa sahihi kutokana na mabadiliko ya kiuchezeshaji wa sheria za FIFA.

Komba alikimbia ndani ya Uwanja wa Mkapa, Julai 3 wakati ubao ukisoma Simba 0-1 Yanga huku mtupiaji akiwa ni Zawad Mauya jambo ambalo lilizua sintofahamu.


Alikuwa ni Clatous Chama kiungo wa Simba aliyesepa na mpira wa shambulizi la kushtukiza kisha alimpa nahodha wake John Bocco ambaye alifanya jaribio lilioishia mikononi mwa Faroukh Shikalo.

Chacha amesema kuwa:”Hapo mwanzo kulikuwa na tabia za mechi kubwa kama ya Simba na Yanga kuwa na waamuzi rundo ambao kazi yao ilikuwa kumsaidia mwamuzi wa kati lakini kwa sasa FIFA wameliona hilo na kuamua kuleta mafunzo mapya.

“Kama mwamuzi wa kati yupo mbali na linafanyika shambulizi la kushtukiza basi mwamuzi msaidizi namba moja au mbili anayekuwa karibu huingia uwanjani kuangalia kila tukio mpaka mwisho wa mpira ili ikitokea sintofahamu ampe usaidizi mwamuzi wa kati.

“Kwenye mataifa mengine hiyo kanuni imeshaanza kufanya kazi hivyo isipokuwa hapa ilikuwa bado hivyo mashabiki wasidhani kwamba Komba alisahau kuingia kukimbia kwenye mstari wake badala yake alilazimika kuingia uwanjani kwa kuwa mwamuzi Emmanuel Mwandembwa alikuwa mbali,” amesema.

Chanzo:Championi.


SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI