Home EURO 2020 ISHU YA UBAGUZI SERIKALI ENGLAND YAPINGA, UCHUNGUZI KUFANYIKA

ISHU YA UBAGUZI SERIKALI ENGLAND YAPINGA, UCHUNGUZI KUFANYIKA


 WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amelaani ubaguzi wa rangi uliojitokeza katika mitandao ya kijamii dhidi ya wachezaji wa England baada ya timu hiyo kupoteza mbele ya Italia katika fainali ya kuwania kombe la Euro 2020.

 

Polisi nchini Uingereza imesema itachunguza matusi na maneno ya ubaguzi wa rangi yaliyoandikwa katika mitandao ya kijamii dhidi ya wachezaji watatu wa England waliolengwa kwenye kadhia hiyo ambao wana asili ya Afrika, Marcus Rashford, Jadon Sancho na Bukayo Saka.

 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Boris Johnson amesema timu ya taifa ya England yapaswa kusifiwa kama mashujaa na si kutupiwa kauli za ubaguzi wa rangi.


 Johnson ameongeza kuwa waliohusika kwa ubaguzi huo wa kushangaza wanapswa kuona aibu wenyewe.


Italia ilishinda kwa penalti 3-2 baada ya muda wa kawaida kukamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

SOMA NA HII  UKRAINE WAPEWA ONYO ISHU YA ULINZI BAADA YA KUPOTEZA KATIKA EURO 2020