Home Yanga SC KAZADI AMTAJA NYOTA ALIYEMSHAWISHI KUJIUNGA YANGA

KAZADI AMTAJA NYOTA ALIYEMSHAWISHI KUJIUNGA YANGA


NYOTA Francis Kazadi Kasengu amesema kuwa Mukoko Tonombe ni moja kati ya watu wanaomshawishi kwa kiasi kikubwa kujiunga na klabu ya Yanga kwa ajili ya msimu ujao.


Kazadi Kasengu na Mukoko 
Tonombe wamewahi kucheza kwa pamoja katika kikosi cha AS Vita lakini kwa sasa wanacheza kwa pamoja katika kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kazadi alisema kuwa amekuwa Akizungumza mara kwa mara na rafiki yake Mukoko Tonombe ambaye amekuwa akimuuliza kuhusu ligi ya Tanzania hususani kuhusu Yanga huku akiweka wazi kuwa kiungo huyo kamshawishi ajiunge na klabu hiyo.


“Mukoko ni rafiki yangu sana, 
tumecheza wote katika klabu ya AS Vita na timu ya taifa ya DR Congo, mara nyingi tumekuwa tukizungumza vitu mbalimbali haswa soka la Tanzania.

 

“Yeye ameniambia anatamani kuniona nikijiunga na Yanga, tulipokutana katika mechi ya timu ya Taifa aliniletea jezi ya Yanga hivyo ninayo jezi ya Yanga na siku zote ananishauri tucheze wote ndani ya Yanga.

 

“Mimi nipo tayari kujiunga na Yanga lakni sitaki kusema nini kinaendelea kwa sasa kwani kila kitu kitakuwa wazi hivi karibuni,”alisema mshambuliaji huyo.

SOMA NA HII  CAF KUAMUA HATMA YA USAJILI SIMBA NA YANGA....MASTAA HAWA HATARINI KUFYEKWA....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here