Home Azam FC KIUNGO MPYA AZAM FC ASEMA AMEKUJA KUCHUKUA MATAJI

KIUNGO MPYA AZAM FC ASEMA AMEKUJA KUCHUKUA MATAJI


 CHARLES Zulu, kiungo mshambuliaji wa Azam FC amesema kuwa amekuja kwa ajili ya kuchukua mataji ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina.

Raia huyo wa Zambia alisaini dili la miaka miwili Julai 4 akitokea Klabu ya Cape Town City ya Afrika Kusini ikiwa ni ingizo jipya ndani ya timu hiyo inayotumia Uwanja wa Azam Complex.

Nyota huyo amesema:”Nina furaha kuwa ndani ya Azam FC kwa kuwa ni moja ya timu bora ninajivunia kwa hilo hasa baada ya kuweza kusaini hapa.

Nimekuja hapa kushinda mataji, nataka kufunga mabao, kutoa pasi za mabao, kwa sababu hiyo ndio kazi yangu ambayo imenifanya niweze kuja hapa,” amesema.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Azam FC ipo nafasi ya tatu na ina jumla ya pointi 64 baada ya kucheza jumla ya mechi 32.


SOMA NA HII  'SOPU' AJILENGESHA TENA KWA MADAKA MISHALE WA YANGA...AFUNGUKA ANAVYOMUOTEAGA..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here