Home Simba SC MAKALI YA SIMBA BONGO NI YALEYALE

MAKALI YA SIMBA BONGO NI YALEYALE


 LICHA ya kukamilisha mzunguko wa pili na kucheza jumla ya mechi 34, safu ya ushambuliaji wa Simba inayoongozwa na John Bocco imeonekana kuwa kwenye makali yaleyale ya msimu wa 2019/20 bila kupoa.

Wakati ikitwaa taji la ligi msimu uliopita baada ya kucheza jumla ya mechi 38, Simba ilifunga jumla ya mabao 78 na kinara wa utupiaji alikuwa ni Meddie Kagere ambaye alitupia mabao 22.

Msimu huu wakiwa wamecheza mechi pungufu ya nne kufikia 38, safu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, raia wa Ufaransa imetupia mabao yaleyale 78 kibindoni na kinara wa utupiaji ni Bocco mwenye mabao 16.

Pia rekodi nyingine ambayo safu ya ulinzi imeweka ni kuruhusu mabao machache ambayo ni 14 tofauti na msimu uliopita ambapo ilikubali kuokota jumla ya mabao 21 nyavuni.

Rekodi pekee ambayo imekuwa ngumu kwa Simba kuvunja ni ile ya kufikisha pointi 88 kwa kuwa msimu huu imekusanya pointi 83.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUFANYA MAKUBWA....MGUNDA AWAPA MTIHANI MZITO MABOSI SIMBA...