Home Yanga SC MZEE MPILI: TULIPASWA KUCHUKUA UBINGWA, SASA MPIRA KIGOMA

MZEE MPILI: TULIPASWA KUCHUKUA UBINGWA, SASA MPIRA KIGOMA


 MZEE wa Yanga ambaye yupo kwenye baraza la Wazee, Mzee Mpili amesema kuwa kwa sasa wapo juu baada ya kuchukua pointi tatu na kituo kinachofuata ni Kigoma.

Yanga inatarajiwa kukutana na Simba kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho inayotarajiwa kuchezwa Julai 25, Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma.

Mpili ambaye alikuwa anatamba tangu awali kwamba Yanga itawafunga Simba ameweka wazi kwamba mpira Yanga upo na kituo kinachofuata ni Kigoma huko hawezi kuwaambia kwa sasa nini kitatokea.

“Matokeo tumeyapata na kama tumeomba matokeo tumepata basi tupo juu leo tumechukua pointi tatu tupo juu na pointi 70 na awali hesabu zetu ilikuwa kuchukua ubingwa.

“Watu wanaona mpira hatuna, sisi ilipaswa tuchukue ubingwa mwaka huu na unaona kwamba kwa sasa tupo juu. Watu ambao nipo nao ni sababu inayofanya tuwe tunajiamini hivyo tusubiri na tuone,” amesema.

Yanga kwenye msimamo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 70 baada ya kucheza mechi 32 Simba ipo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 73 baada ya kucheza mechi 30.

SOMA NA HII  KUHUSU TETESI ZA KUTUA SIMBA....BANGALA AANIKA MSIMAMO WAKE NA YANGA...NABI ATAJWA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here