Home Namungo FC NAMUNGO FC HESABU ZAO KWA RUVU SHOOTING ZIPO HIVI

NAMUNGO FC HESABU ZAO KWA RUVU SHOOTING ZIPO HIVI


 KINDAMBA Namlia, Ofisa Habari wa Namungo FC ya Lindi ameweka wazi kwamba mchezo wao wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting watapambana kusepa na pointi tatu muhimu.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 32 ipo nafasi ya 5 kibindoni ina pointi 43 inakutana na Ruvu Shooting iliyo nafasi ya 10 na pointi 38.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mabatini majira ya saa 10:00 jioni huku ukitarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Ruvu wao wanahitaji pointi tatu kwa kuwa hawana uhakika wa kubaki ndani ya ligi ikiwa watapoteza kwa sababu pointi ambazo wanazo zinaweza kufikiwa na Gwambina FC iliyo nafasi ya 16 na pointi zake 34 baada ya kucheza mechi 32.

Namlia amesema:”Kila kitu kipo sawa, wachezaji wanajua kwamba tunahitaji pointi tatu kikubwa mashaibiki wazidi kutupa sapoti.

“Jambo la msingi ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu hivyo hakuna kazi ambayo tutakwenda kufanya zaidi ya kusaka pointi tatu,” amesema.

namungo inapambana kupata pointi tatu kufufua matumaini ya kumaliza nafasi ya nne ili ipate zali la kuiwakilisha nchi kimataifa kwa sababu kuna nafasi nne kwa Tanzania.

Ugumu upo kutokana na wamiliki wa nafasi hiyo kwa sasa ni Biashara United pointi zao kibindoni ni 49.

SOMA NA HII  LUSAJO: - MSINISHINDANISHE NA MAYELE...MNANIPA PRESHA...,UNAWEZA UKAPATA MAJERAHA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here