Home kimataifa RASHFORD MAJANGA, KUFANYIWA UPASUAJI WA BEGA

RASHFORD MAJANGA, KUFANYIWA UPASUAJI WA BEGA


 MSHAMBULIAJI wa Manchester United, raia wa England, Marcus Rashford anatarajiwa kukaa nje ya uwanja mpaka Oktoba akijiandaa kufanyiwa upasuaji wa bega.

Nyota huyo anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa bega muda wowote kuanzia sasa hivyo hataonekana ndani ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu.

Tatizo la bega kwa nyota huyo lilianza kumsumbua tangu mwaka jana lakini hakuweza kufanyiwa upasuaji kwa mujibu wa vipimo ambavyo amefanya hivi karibuni ameambiwa kwamba anatakiwa kufanyiwa upasuaji ili apewe matibabu ya haraka.

Ikiwa itakuwa hivyo nyota huyo atazikosa mechi tisa ndani ya Ligi Kuu England na tatu za Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu huu wa 2021/22.

SOMA NA HII  RONALDO AFIKISHA JUMLA YA HAT TRICK 58

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here