Home Yanga SC SENZO: TUNA JAMBO LETU KIGOMA

SENZO: TUNA JAMBO LETU KIGOMA


MSHAURI mkuu wa masuala ya mabadiliko ndani ya kikosi cha Yanga, Senzo Mbatha amefunguka kuwa wana jambo lao mkoani Kigoma, la kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wa fainali ya kombe la Shirikisho.

Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana katika fainali ya kombe la Shirikisho, itakayochezwa katika uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma Julai 25, mwaka huu.

Huu utakuwa mchezo wa nne kwa Simba na Yanga kukutana msimu huu, ambapo Yanga itaingia katika mchezo huo ikiwa na rekodi nzuri katika michezo mitatu mfululizo iliyopita, ambapo Yanga wameshinda michezo miwili (Fainali ya mapinduzi na mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu), huku mchezo wa mzunguko wa kwanza ukimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Akizungumzia maandalizi yao, Senzo amesema: “Tunajivunia mafanikio ambayo tumekuwa nayo kama timu, hasa baada ya kupitia vipindi vigumu, lakini kikosi chetu kinaonekana kuimarika kila siku kama yalivyo malengo yetu.

“Tumesaliwa na michezo miwili kwenye Ligi Kuu Bara, ni lazima tuhakikishe tunamaliza katika nafasi nzuri, baada ya hapo tutasubiri maelekezo ya kocha Nabi juu ya mipango ya kujiandaa na fainali kwani kuna jambo la kumalizia Kigoma.”

SOMA NA HII  WAKATI TFF WAKIMRUDISHA YANGA...FIFA KUMPA KIBALI FEI TOTO CHA KUCHEZA POPOTE...