Home Yanga SC SIKU MOJA KABLA YA DERBY :NIYONZIMA, LAMIRE, SARPONG WAFUKUZWA KAMBINI

SIKU MOJA KABLA YA DERBY :NIYONZIMA, LAMIRE, SARPONG WAFUKUZWA KAMBINI


SOKA LA BONGO linajua kwamba Kocha Nabi Mohammed wa Yanga, amewaambia viongozi jana kwamba Haruna Niyonzima na Lamine Moro hataki kuwaona kambini kuelekea mechi ya Jumamosi dhidi ya Simba.

Nabi amefanya maamuzi hayo magumu baada ya wachezaji hao kuchelewa kuripoti kambini huku kiufundi wakiwa wamepoteza pia namba kwenye kikosi cha kwanza hivikaribuni.

Mbali na hao pia Soka la Bongo linajua kwamba Nabi amewaondoa Michael Sarpong kwa sababu za kinidhamu na Balama Mapinduzi, Yassin Mustafa ambao ni majeruhi.

Habari za uhakika zinasema kwamba Yanga walirejea kambini Jumatatu lakini Haruna na Lamine hawakurejea na hakukuwa na sababu mpaka jana alipowaambia viongozi kwamba hataki kuwasikia watu hao wala sababu zao zozote walizonazo.

Licha ya viongozi wa Yanga kukwepa kulitolea ufafanuzi sakata hilo, Soka la Bongo limejiridhisha pia amewaambia hata wakiweza wafanye uamuzi wa zaidi ya mechi hiyo kwani hawapo tena kwenye programu yake. 

Soka la Bongo linajua kwamba Nabi atawatema mastaa wa kigeni kwenye usajili ujao akiwemo Haruna, Lamine, Sarpong, Fiston Abdulrazak,Carlihnos ambaye ameshasepa na kipa Mkenya, Faroukh Shikalo.

Katika hatua nyingine, jana kulikuwa na kikao kizito cha viongozi wa matawi kwenye makao makuu ya Yanga Jangwani ili kuweka sawa ishu ya mechi ya watani.

SOMA NA HII  RIVERS UNITED WAZIDIWA KETE NA YANGA...WACHACHAWA! WAPAGAWA!...ISHU NZIMA IKO HIVI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here