Home Simba SC WATANO SIMBA WAINGIA KIKOSI CHA KWANZA

WATANO SIMBA WAINGIA KIKOSI CHA KWANZA


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wote ni muhimu kwenye kikosi hicho jambo ambalo linampa furaha pale wanapofanya vizuri.

Jana, Julai 11 kikosi cha kwanza ambacho kilianza mbele ya Coastal Union kilikuwa na mabadiliko ya wachezaji watano ambao walikuwa hawapati nafasi katika mechi nyingi kutokana na ushindani wa namba.

Nyota hao ni pamoja na Kened Juma, Beno Kakolanya, Gadiel Michael, David Kameta na Ibrahim Ame ambao waliyeyusha dk 90 pia Said Ndemla naye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Clatous Chama.

Gomes amesema kuwa kila siku amekuwa akifurahia maendeleo ya wachezaji wake kutokana na uwezo ambao wanao.

“Kuna wachezaji wengi wazuri ambao wanafanya kazi kwa ushirikiano hilo ni jambo jema kwangu na timu kiujumla.

“Kila mmoja ana nafasi ya kucheza na kwa mechi ambazo zimebaki nina amini kwamba wale ambao walikuwa hawapati nafasi itakuwa ni zamu yao kuonekana kwani kila mchezaji ninajua uwezo wake.

“Yupo Said Ndemla, Miraj Athuman pamoja na Gadiel Michael wote wapo vizuri ni suala la muda wao kuonyesha kile ambacho wanaweza,” amesema.

Kwenye msimamo Simba ni nafasi ya kwanza na pointi zao ni 79 baada ya kucheza jumla mechi 32 wanafuatiwa na Yanga nafasi ya pili na pointi 70.

Mchezo wao ujao wa ligi ni dhidi ya Azam FC unatarajiwa kuchezwa Julai 15, Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  SIMBA WAIFANYIA UMAFIA ASEC...MO DEWJI ATUA KAMBINI...RAIS SAMIA AHUSISHWA KWENYE MCHAKATO...