Home Yanga SC YANGA YATAMBA KUIFUNGA SIMBA KWA MKAPA

YANGA YATAMBA KUIFUNGA SIMBA KWA MKAPA

 “NJIA pekee ya kubadili Simba asiwe katika hali hiyo ni kukata mkia wake ili asionekane mjini, na tunaamini kwamba sisi Yanga tunakwenda kumkalisha mnyama taratibu, mashabiki msiogope njooni kwa Mkapa,” kauli ya kibabe kutoka kwa Haji Salum, marufu kama Mboto. 


Tayari kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Julai 3.


Mboto ameongeza kuwa wanaskia maneno mengi kutoka kwa watani zao wa jadi ila wao hawataongea watafanya kazi kwa vitendo.


Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes inahitaji pointi tatu ili kutangazwa kuwa mabingwa huku Yanga ya Nabi ikiwania nafasi ya pili na kuhitaji kufufua matumaini ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara lililo mikononi mwa Simba.


Ukitazama msimamo Yanga ipo nafasi ya pili ina pointi 67 na Simba ni inaongoza ikiwa na pointi 73 msimu wa 2020/21.

Simba imecheza jumla ya mechi 29 imefunga mabao 69 na Yanga imecheza jumla ya mechi 31 imefunga jumla ya mabao 49.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO....NABI ASHTUKIA JAMBO ZITO YANGA....KAMBI YA AZAM YACHUNGUZWA KIJASUSI...