news

KAGERA SUGAR:TUTAFANYA USAJILI MZURI KUFIKIA MALENGO

admin August 5, 2021 12:43 pm


 FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa watafanya usajili mzuri kwa msimu wa 2021/22 ili waweze kufikia malengo ambayo wanahitaji.

Msimu huu Kagera Sugar imemaliza ikiwa nafasi ya 12 na pointi 40 baada ya kucheza mechi 34 na ilikuwa inapambana kwenye kujinasua kushuka daraja jambo ambalo lilifanikiwa.

Tayari panga limepita ndani ya timu hiyo inayotumia Uwanja wa Kaitaba kwa wachezaji nane kuachwa mazima ikiwa ni pamoja na Mohamed Ibrahim, Ally Mtoni pamoja na kipa Benedict Tinocco.

Baraza amesema:”Nilikuja hapa Kagera Sugar ili kuonyesha ubora ambao ninao na sikuwa na mashaka kwa kuwa nilikuwa ndani ya Biashara United na nilifanya vizuri pia.

“Kwa ajili ya wakati ujao imani yangu ni kuona kwamba tunafanya usajili vizuri kwa kuwa kila mmoja anahitaji kuona timu inafanya vizuri hasa kwenye mashindano.

“Katika wakati wa usajili tutafanya kazi kubwa ya kusajili wachezaji wazuri ambao watakuwa na kazi ya kusaka ushindi ndani ya uwanja,” .

Tayri nyota wao ambaye alikuwa kinara kwenye utupiaji ni Yusuph Mhilu, yupo zake ndani ya Simba akiwa amepewa dili la miaka miwili.

AZAM FC KAZINI TENA LEO KOMBE LA KAGAME AZAM FC BADO IPO CHIMBO KUSHUSHA MAJEMBE YA KAZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply