Home news BAADA YA KUBWAGA MANYANGA, MANARA KUZUNGUMZA LEO

BAADA YA KUBWAGA MANYANGA, MANARA KUZUNGUMZA LEO


 LEO Agosti 8,2021 aliyekuwa Ofisa Habari wa Simba Haji Manara ataogea na aandishi wa Habari pamoja na jamii kiujumla kwa lengo la kuwashukuru Wanasimba.

Manara alibwaga manyanga ndani ya Simba baada ya kufanya kazi kwa mafanikio makubwa na sababu kubwa ya yeye kubwaga manyanga haikuwekwa wazi na mabosi wa Simba.

Kupitia katika Ukurasa rasmi wa Instagram wa Haji Manara ameandika:”Kupitia Wanahabari leo tarehe 4/8/2021 saa tano asubuhi nitaongea na kuwashukuru Watanzania na Wanasimba kwa kunipa nafasi ya kuwatumikia mabingwa wa nchi.


“Heshima mliyonipa nnao wajibu wa kuwashukuru na kusema asante kwenu,ninao pia wajibu wa kushukuru taasisi nyingine zote tulizofanya kazi pamoja.

“Mkutano huu utarushwa live na page hii, (Haji Manara) Manara Tv na Azam Tv,”.


Ilikuwa ni Julai 28 taarifa ya kusepa Simba ilipotolewa na mbadala wake aliyetangazwa ni Ezekiel Kamwaga. 
SOMA NA HII  KUHUSU SIMBA KUFUZU ROBO FAINALI CAF...BARBARA KACHEEKAA..KISHA AKASEMA HAYA..