Home news BAADA YA KUTEMWA AS VITA…PILAU NA BIRIAN VYAMRUDISHA TSHISHIMBI BONGO

BAADA YA KUTEMWA AS VITA…PILAU NA BIRIAN VYAMRUDISHA TSHISHIMBI BONGO


NAHODHA wa zamani wa Yanga, Papy Tshishimbi amethibitisha mapenzi yake na Tanzania baada ya kurudi tena kula maisha baada ya kumaliza mkataba na AS Vita.

Tshishimbi alishawahi kulithibitishia Soka la Bongo Blog kuwa anaipenda Tanzania na anatamani kubadili uraia wake kutoka DR Congo na kuwa Mtanzania.

Amesema yupo Tanzania kwaajili ya maisha yake binafsi na sio jambo lolote linalohusu soka na kubainisha kuwa ameamua kuachana na soka.

“Nipo nchini hapa lakini hakuna ishu yoyote iliyonileta kuhusu mpira nimekuja tu kutembea kwasababu ni nchi ambayo naipenda na nilikaa kwa muda mrefu na kupewa ushirikiano mzuri,” alisema.

Awali akihojiwa na moja ya chombo cha habari, Tshishimbi alifunguka kuwa mbali na mazingira ya Tanzania, pia anapenda sana vyakula vinavyopikwa hapa, ikiwemo biriani na pilau, hivyo pengine pia hii ikawa sababu ya kumfanya kurudi nchini.

SOMA NA HII  WAKATI MASHABIKI WAKISUBIRI 'THANK YOU' YA ONYANGO...AHMED ALLY KAAANIKA JAMBO LILIVYO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here