Home Namungo FC BAADA YA KUTEMWA AZAM FC OBREY CHIRWA HUYOOO NAMUNGO FC

BAADA YA KUTEMWA AZAM FC OBREY CHIRWA HUYOOO NAMUNGO FC


Mshambuliaji wa zamani wa klabu za Young Africans na Azam FC Obrey Chirwa, huenda akaibukia Namungo FC, baada ya kuachwa huko Azam Complex Chamazi, mwezi Julai.

Chirwa alikua miongoni mwa wa wachezaji waliofungashiwa virago Azam FC, na nafasi zao kujazwa na wachezaji wengine katika kipindi hiki cha usajili wa kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa 2021/22.

Klabu ya Namungo FC inatajwa kuanza mazungumzo na Mshambuliaji huyo, huku wakiwa na matumaini makubwa ya kumsajili kwenye kikosi chao.

Taarifa kutoka ndani ya Namungo FC zinasema kuwa, viongozi wa klabu hiyo ya mkoani Lindi wako kwenye hatua za mwisho kuinasa saini ya mshambuliaji huyo ambaye alifunga mabao 5 msimu uliopita.

Endapo mazungumzo ya pande hizo mbili yatakamilika, Chirwa atajiunga na Namungo FC kama mchezaji huru, kufuatia mkataba wake na Azam FC kufikia kikomo mwishoni mwa msimu uliopita.

SOMA NA HII  YANGA vs NAMUNGO...MECHI 'MFUPA MGUMU' KWA YANGA....HAWAJAWAHI KUPATA USHINDI DHIDI YA NAMUNGO..