Home Yanga SC BREAKING: YANGA YAMALIZANA NA BEKI KISIKI WA KAZI

BREAKING: YANGA YAMALIZANA NA BEKI KISIKI WA KAZI


WAMEJIBU ghafla mabosi wa Yanga baada ya muda mfupi watani zao wa jadi kumtambulishwa Sadio Kanoute hawajapoa kwa kuwa wameachia nao mashine ya kazi.

Anaitwa Yanick Bangala Litombo ambaye ametambulishwa leo rasmi kupitia ukurasa rasmi wa Yanga kwa maneno mafupi kwamba, “Bangala is Green and Yellow’) (Bangala ni kijani na njano).

 Kwa sasa Yanga wapo zao nchini Morocco ambapo wameweka kambi ya muda wa siku 10 na huyu mchezaji wao wa leo anakuwa wa 11 kutambulishwa baada ya wale wengine Wacongo waliotambulishwa ikiwa ni pamoja na Heritier Makambo, Fiston Mayele na Djuma Shaban.


Kwa mujibu wa Kaimu Katibu wa Yanga, Haji Mfikirwa amebainisha kwamba wachezaji wote ambao wamesajiliwa pamoja na mipango kazi itazinduliwa rasmi Agosti 29.

Siku hiyo itakuwa ni siku ya kilele cha Mwananchi hivyo majembe yote ya kazi ikiwa ni pamoja na mzawa Dickson Ambundo naye atatambulishwa pia.


Inatajwa kuwa dili ambalo amesaini ni miaka miwili kwa ajili ya msimu wa 2021/22.


SOMA NA HII  KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA ZANACO, KILELE CHA WIKI YA MWANANCHI