Home kimataifa CITY KUMPA DILI KANE

CITY KUMPA DILI KANE


MABOSI wa Manchester City wameanza mazungumzo na wamiliki wa mchezaji Harry Kane ambao ni Tottenham kwa ajili ya kukamilisha dili la usajili wa nyota huyo.

Manchester City wamedhamiria kuipata saini ya mshambuliaji Kane jambo ambalo limewafanya wazidi kulikomalia dili hilo kwa muda mrefu ili kuwa naye katika msimu wa 2021/22 ambao tayari umeanza kurindima na kwenye mchezo wa ufunguzi, ubao wa Uwanja wa Brentford Comunity ulisoma Brentford 2-0 Arsenal.

Tayari Kane amewaambia mabosi zake kwamba anataka kuondoka hapo ili apate changamoto mpya jambo ambalo linaongeza nafasi kwa dili lake kukamilika ikiwa maongezi yatakwenda sawa.

Awali dau lake lilikuwa linatajwa kuwa pauni milioni 150 ila likashushwa mpaka pauni milioni 120 hivyo bado wanazungumza ili kukamilisha dili hilo na huenda kesho Jumapili mambo yakawa yamejibu na nahodha huyo wa timu ya taifa ya England anaweza kuwa mali ya City.

SOMA NA HII  CORONA YAITIKISA MANCHESTER UNITED

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here