Home Azam FC JITIHADA ZA AZAM FC ZAKWAMIA AZAM COMPLEX, KAGAME CUP

JITIHADA ZA AZAM FC ZAKWAMIA AZAM COMPLEX, KAGAME CUP

 JITIHADA za vijana wa Azam FC waliokuwa wananolewa na Kocha Msaidizi,  Vivier Bahati katika kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Kagame, ziligonga mwamba jana Agosti 11.

Ni katika mchezo wa nusu fainali iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex,  dakika 90 za awali zilimeguka ngoma ikiwa Azam FC 2-2 Big Bullets. 

Bao la mapema la Bright Muthalk dk ya kwanza liliwapoteza wawakilishi wa Tanzania,  Azam FC waliokubali kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao hilo.

Kipindi cha pili waliamka Azam FC na kutengeneza majaribio kadhaa na iliwabidi wasubiri mpaka dk ya 67 kupachika bao la usawa kupitia kwa Paul Peter. 

Kasi ilizidi kuwa kubwa kwa vijana hao ambapo dk ya 74 nyota wao mwingine Oscar Masai alipachika bao la pili kwa Azam FC.

Bao hilo lilidumu dk mbili pekee kwa kuwa makosa ya safu ya ulinzi yalimpa manufaa Bright tena akapachika bao la usawa dk 76 na kufanya ubao wa Azam Complex kusoma Azam FC 2-2 Big Bullets. 

Zilipoongezea dk 30 hakukuwa na mbabe na Azam FC ilitolewa katika changamoto ya penalti ambaoo ilishinda 2-4 Big Bullets ambao watacheza fainali Jumamosi na Express ambao waliwatoa KMKM.

SOMA NA HII  DUBE KUIBUKIA MAJIMAJI KUWAVAA SIMBA LEO