Aliyekuwa msemaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, Haji Sunday Ramadhan Manara, kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusu aliyerithi mikoba yake kwa muda ndani ya klabu hiyo.
Simba SC ilimtangaza Ezekiel Kamwaga kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino kwa muda ndani ya klabu hiyo, baada ya kuachana na Haji Manara mwishoni mwa mwezi Julai.
SOMA PIA: ACHANA NA BILIONI 20..,HAPA TU NDIPO MO DEWJI ALIPOWASHIKA SIMBA SC
Manara ambaye kwa sasa yupo nje ya nchi, amesema wadau wa soka la Bongo hawapaswi kumfananisha na Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari ya Simba SC Ezekiel Kamwaga kwa sababu kila mtu anastahili yake ya usemaji.
Manara amesisitiza kuwa, Kamwaga anaujua mpira na ni mwandishi wa habari mzuri na msomi kwa hiyo anaimani ataitendea haki nafasi hiyo aliyopewa simba SC, japo itamchukua muda mrefu kuwa vile wanasimba wanataka Kamwaga awe.
Manara amesema Haji atabaki kuwa Haji na Kamwaga pia atabaki kuwa Kamwaga, hawawezi kufanana hivyo wanasimba wasitarajie Kamwaga atakua na staili ileile kama ya Haji.
SOMA PIA: SIMBA WATIA TIMU MOROCCO KWA AJILI YA KAMBI
Kamwaga aliwahi kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya klabu ya Simba SC wakati wa Uongozi wa Ismail Aden Rage, na kisha alipandishwa cheo hadi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, kabla ya kuondolewa siku chache baada ya utawala wa Evance Aveva kuingia madarakani.