Home Yanga SC MANARA ATUPA KOMBORA LINGINE MSIMBAZI…AFUNGUKA KUHUSU KUWA MKUBWA KULIKO SIMBA

MANARA ATUPA KOMBORA LINGINE MSIMBAZI…AFUNGUKA KUHUSU KUWA MKUBWA KULIKO SIMBA


Mwanafamilia mpya wa Young Africans Haji Sunday Manara ameushambuliua Uongozi wa Simba SC kwa mara nyingine, kwa kusema bado ana mengi ya kusema kuihusu klabu hiyo.

Manara amefunguka hayo alipohojiwa Wasafi FM kupitia kipindi cha Sports Arena, ambapo amesema yeye ni muumini wa kuweka kumbukumbu wa mambo aliyofanyiwa, na kama atalazimika kuyasema atayasema.

“Ukitafuta Wanaadamu 10 wastahimilivu Duniani na Mimi ntakuwemo Ila Mimi hata uwe Mkubwa Vipi una hela Kama Bilgate sikuogopi Hata Uwe na Mihela unajaza Dunia Nzima Lakini Penye Ukweli Ntasema”amesema Haji.

Mdau huyo wa soka la Bongo ambaye juzi Jumanne (Agosti 12) aliushtua umma kwa kuhamia Young Africans, ameshangazwa sana na kauli za baadhi ya viongozi wa Simba SC na baadhi ya wanachama kusema alikua anajitutumua na kujiona ni zaidi ya klabu hiyo, jambo ambalo hakuwahi kulifanya hata siku moja ya masiha yake huko Msimbazi.

“Nimeondoka Baadae Wanaanza kusema Kuwa Simba Ni kubwa Kuliko Mtu yeyote Jamani Mimi niliwahi kusema wapi kwamba ni Mkubwa Kuliko Simba Ebu Tafuta Hiyo Clip Popote uilete Hapa”

“Na Bahati Mbaya wakaanza kuwatumia Watu Ambao nawajua kunichafua, Nilitengeneza Team ya Propaganda ili kuwashuhulikia Yanga baadae Ile timu Ndio wanakutumia kunichafua, Yani kinyago nimekichonga Mimi mwenyewe ndo kinishuhulikie.” amesema Haji.

Haji Manara anatarajiwa kuwa Mshehereshaji (MC) katika Tamasha la Siku ya Mwananchi litakalofanyika Jumapili (Agosti 29) Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

SOMA NA HII  BAADA YA YACOUBA KUWEKWA KANDO.... HIKI HAPA KIFAA CHA TP MAZEMBE KINACHOKUJA YANGA...