Home kimataifa MANCHESTER UNITED YAFUNGUA LIGI KWA KISHINDO, YATEMBEZA 5 G

MANCHESTER UNITED YAFUNGUA LIGI KWA KISHINDO, YATEMBEZA 5 G


MANCHESTER United leo wamefungua Ligi Kuu England kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya wapinzani wao Leeds katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Old Trafford.

 Nyota wao Bruno Fernandes alitupia mabao matatu na kusepa na mpira wake aliyafunga mabao hayo dakika ya 30, 54 na 60 huku wengine wakiwa ni Mason Greenwood dk 52 na Fred dk 68 waliimaliza jumla Leeds.


Luke Ayling huyu alipachika bao pekee la kufutia machozi kwa Leeds ilikuwa dk 48 ambapo aliwafanya waamini wangeweza kugawana pointi moja ila mambo yakawa tofauti.

Amechaguliwa kuwa nyota wa mchezo wa leo Pogba kutokana na uwezo ambao ameuonyesha ndani ya uwanja.

Nyota Paul Pogba ameweza kuwa wa moto leo ndani ya uwanja mbele ya mashabiki wapatao 75,000 ambapo aliweza kutoa jumla ya pasi nne za mabao.

SOMA NA HII  UBAGUZI WA RANGI WAMUONDOA GWIJI THIERY HENRY KWENYE MITANDAO YA KIJAMII