Home Yanga SC PAMOJA NA KUFANYA VIBAYA AKIWA NA YANGA..FARID MUSA ATAJWA NA STAR WA...

PAMOJA NA KUFANYA VIBAYA AKIWA NA YANGA..FARID MUSA ATAJWA NA STAR WA MOROCCO


WINGA Simon Msuva yuko hapa nchini Morocco akijiandaa na msimu mpya wa ligi akiwa na klabu yake bingwa wa nchi hii, Wydad Athletic lakini aliposikia Yanga ipo hapa akamkumbuka winga mwenzake mmoja kisha akampa ushauri.

Ushauri wa Msuva umetua kwa winga wa kushoto wa timu yake ya zamani Yanga akimwambia anajua kwamba alikuwa na msimu wa kwanza mgumu ndani ya Yanga, lakini wala hilo lisimsumbue.

Msuva amenukuliwa na gazeti la  Mwanaspoti kwamba anafuatilia soka la Tanzania hususani klabu yake ya zamani Yanga na anajua kwamba Farid amekuwa akikutana na wakati mgumu kidogo kufanya vyema.

“Nafuatuilia soka la Tanzania na mtu kama Farid pale Yanga najua tangu atoke Hispania hajawa na wakati mzuri tofauti na watu walichotarajia lakini nataka nimwambie bado ana wakati mzuri wa kufanya vizuri ndani ya Yanga,” alisema Msuva.

Mshambuliaji huyo alisema kuwa Farid wala asidhani kama amekumbana na wakati mgumu ndanio ya Yanga na kwamba anachotakiwa kufanya ni kuongeza juhudi uwanjani kwa kupambana.

Alisema yeye alikumbana na wakati mgumu zaidi alipokuwa Yanga akizomewa na mashabiki lakini bado aliongeza juhudi na baadaye akawa shuijaa ndani ya kikosi hicho.

“Farid anatakiwa kwanza kujua mashabiki wa timu yake, bado hajakutana na wakati mgumu namkumbusha maisha yangu mimi Simon nilipokuwa Yanga kila wakati nilikuwa nazomewa. Ila sikutoka mchezoni niliwaasikiliza makocha wanataka nini,nilijituma binafsi na unajua mashabiki sio kwamba wanakuchukia wanafanya vile ili ufanye vizuri.”

SOMA NA HII  MTUNISIA MWINGINE ASHUSHWA YANGA KUMWAGA WINO