Home Simba SC PAMOJA NA UWEZO MKUBWA..JOASH ONYANGO NAYE ATEMWA…MAJEMBE HAYA KUCHUKUA NAFASI YAKE

PAMOJA NA UWEZO MKUBWA..JOASH ONYANGO NAYE ATEMWA…MAJEMBE HAYA KUCHUKUA NAFASI YAKE


BEKI Joseph Onyango wa Simba hajajumuishwa katika kikosi cha timu ya Taifa Kenya kinachotarajia kucheza mechi za kufuzu fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Qatar 2022.

Onyango ambaye amejihakikishia nafasi katika kikosi cha Simba, awali alikuwa anapata nafasi kwenye timu ya Taifa lakini lakini safari hii ameachwa kwenye mechi za kuwania nafasi ya kucheza kombe la Dunia.

Mabeki walioitwa Joseph Okumu (KAA Gent, Belgium), Eric Ouma (AIK, Sweden), Eugene Asike (Tuskere), Nashon Alembi (KCB), Harun Shakava (Gor Mahia), Andrew Juma (Gor Mahia), Siraj Mohamed (Bandari) na Clyde Senaji (AFC leopards).

Wengine ni Frank Odhiambo  (Gor Mahia), Bolton Omwenga (Nairobi City Stars), Daniel Sakari (Kariobangi Sharks) na Baraka Badi (KCB).

Viungo ni Richard Odada (Red Star Belgrade, Serbia), Duke Abuya (Nkana, Zambia), Duncan Otieno (Lusaka Warriors, Zambia), Lawrence Juma (Sofapaka), Kenneth Mguna (Azam Fc,TZ), Kevin Kimani (Wazito) na Patillah Omoto (Kariobangi Sharks).

Wengine ni Enock Momanyi (FC Talanta), Jackson Macharia (Tusker), Eric Johanna (Jonkopings Sondra IF, Sweden), Boniface Muchiri (Tusker) na Abdallah Hassan (Bandari).

Upande wa washambuliaji walioitwa ni Michael Olunga (Al-Duhail, Qatar), Masud Juma (Difaa El Jadid, Morocco), Cliffton Miheso (Gor Mahia), Erick Kapaito (Kariobangi Sharks), Elvis Rupia (AFC Leopards), Samuel Onyango (Gor Mahia) na Benson Omalla (Gor Mahia)

Makipa walioitwa ni Ian Otieno (Zesco Utd, Zambia), James Saruni (Ulinzi Stars), Joseph Okoth (KCB), Brian Bwire (Kariobangi Sharks) na Brandon Obiero(Kariobangi Sharks).

SOMA NA HII  GOMES 'AKUNWA' NA 'KOMBINESHENI' YA MUGALU NA BOCCO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here