Home Simba SC RASMI, ISRAEL MWENDA NI MALI YA SIMBA

RASMI, ISRAEL MWENDA NI MALI YA SIMBA

 


ISRAEL Mwenda, beki wa kulia kutoka Klabu ya KMC kwa sasa ni mali ya Simba baada ya kutambulishwa rasmi leo Agosti 16.

Nyota huyo alikuwa nahodha katika timu ya taifa ya Tanzania chini ya miaka 23 iliyotwaa taji la Cecafa Challenge 2021 nchini Ethiopia.

Akizungumza baada ya kutambulishwa leo beki huyo amesema kuwa atapambana kwa ajili ya kuipa mafanikio timu hiyo.

“Nitapambana kwa ajili ya kuipa mafanikio timu yangu kwa kuipa mataji pamoja na ushindi kwa kuwa malengo ni kuona kwamba tunafikia malengo.

“Kila ambapo ninapata nafasi nimekuwa nikipambana ili kufanya vizuri hivyo kwa kuwa nipo kwenye changamoto mpya basi nitashirikiana na wengine, “. 

Simba imeweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2021/22. Nyota huyo inatajwa kuwa amesaini dili la miaka miwili.

SOMA NA HII  SIMBA KUYAKOSA MABAO 42 NDANI YA LIGI KUU BARA MAZIMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here