Home Makala USAJILI UKIWA WAKUKURUPUKA, ITAFAHAMIKA TU LIGI IKIANZA

USAJILI UKIWA WAKUKURUPUKA, ITAFAHAMIKA TU LIGI IKIANZA


 HAKUNA namna kwa sasa kila timu inavutia kwake na ikitamba kufanya usajili makini. Hili ni sawa na kila mmoja anastahili kupongezwa kwa kile ambacho anakifanya.

Katika vitu ambavyo huwa havitaki ubishi ni muda, ukifika kila kitu kinakuwa bayana yale madudu yote ambayo yalikuwa yanafichwa yataonekana.

Namna ambavyo kila timu inaingia sokoni na kusajili wachezaji inaowataka itafahamika tu wakati ukifika. Mashabiki watajua kwamba usajili ulikuwa ni pendekezo la mwalimu ama suala la kukurupuka.

Wapo wachezaji waliouzwa na walionunuliwa na katika hayo yote yatafahamika muda unakuja. Unaambiwa unaweza kuwadanya watu wote ila sio kila wakati ni jambo la kusubiri.

Pale ngoma itakapoanza kudunda uwanjani kwa kasi huku kila timu ikiwa  inapambania kufikia malengo ambayo imejiwekea kila kitu kitakuwa wazi.

Nina uhakika kwamba zipo timu ambazo hazina uhakika wa kuwa na nguvu ya kushindana katika mechi za mwanzo kwa kuwa kutakuwa na ugeni wa wachezaji ila wanakomaa kuwa wapo vizuri ni sawa. 

Ugumu haupo kwa timu pekee bali hata wachezaji nao wana kazi kubwa ya kufanya kutimiza majukumu yao pale ambapo wanapewa kazi ya kufanya.

Kwa sasa wakati wa maandalizi wachezaji wanajukumu la kutengeneza mpango kazi wao huku wakiwatazama wale  ambao waliweza kupata ofa nzuri na wengine kuongezewa mikataba ila yote itatokana na jitihada zao.

Kitu cha msingi kwa sasa kila mmoja kutazama namna ambayo kwake ni bora katika kutimiza majukumu bila kumuumiza mwingine kwa kuwa hakuna namna ya kukwepa matokeo ya uwanjani.

 Wachezaji katika mechi za ufunguzi wana kazi ya kuanza kujenga hali ya kujiamini ambayo itawapa nguvu ya kufanya vizuri.Uzuri ni kwamba namna utakavyoanza ndivyo utakavyomaliza hivyo muhimu kujipanga bila kuchoka.

Msingi kwa wachezaji kwenye mechi hizi za ufunguzi wajitahidi kutumia akili nyingi uwanjani kuliko kutumia nguvu kwa sababu kwa kutumia nguvu nyingi kutayeyusha ndoto za wengine ambao wanaweza kupata majeraha.

Ambazo zimepanda daraja zinapaswa zitambue kwamba ushindani ndani ya ligi ni mkubwa na kila timu inahitaji kupata ushindi ili kufikia malengo.

Zile ambazo zimeshindwa kupanda kwa msimu huu wakati wao upo msimu ujao zinapaswa kupambana kufikia malengo yao.

Ipo wazi kwamba kila timu inahitaji kupata matokeo na kwa kuwa kuna dirisha la usajili basi wachezaji wamekuwa wakionyesha uwezo wao huku wakati mwingine wakihatarisha maisha yao na ya wachezaji wengine. 

Basi kinachotakiwa kwa sasa ni kuwa makini kwenye kila hatua kwa wachezaji pamoja na wamiliki za timu. Kikubwa ni maandalizi mazuri na hesabu za msimu mpya.

Ikiwa timu itaanza kuboronga hapo majibu ya usajili taratibu yataanza kuonekana. Ikiwa mpaka mzunguko wa pili utafika mambo ni magumu hapo kila kitu kitakuwa wazi na kila mmoja atajua kwamba alikuwa na wachezaji wa aina gani.

SOMA NA HII  KUNA MIKOA SUGU KWA KUSHUSHA NA KUPANDISHA TIMU LAZIMA IBADILIKE

 Kwa zile ambazo zimetoka kupanda msimu huu ambazo ni mbili zimepanda moja kwa moja Geita Gold na Mbeya Kwanza basi zinakaribishwa kwenye ulimwengu wa ligi kuu.

Kikubwa kinachohitajika ni maandalizi makini na kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa wakati sahihi jambo hili litaongeza ushindani na kuleta matokeo mazuri.

Mara nyingi tumeshuhudia timu kuanza kuonyesha ushindani mkubwa kwenye mechi zao za awali ama msimu wa kwanza mwisho wa siku zinaangukia pua msimu unaofuata.

Zile ambazo zinapanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza zina kazi kubwa ya kuanza kufanya maandalizi ili ziweze kuleta ushindani wa kweli ndani ya ligi.

Kila kitu kinawezekana ikiwa kutakuwa na mpango makini na ukweli ni kwamba kupanda ni rahisi na kushuka ni rahisi pia lakini ukishashuka kurudi huku juu huwa inakuwa ngumu.

Zile ambazo zimeshuka daraja zimekuwa zikipambana kwa muda mrefu kuweza kurudi ndani ya Ligi Kuu Bara. Hii inatokana na utofauti na kuwa kwenye changamoto tofauti katika Ligi Daraja la Kwanza.

 Kupitia zile ambazo zilishuka daraja baada ya kupanda basi iwe funzo kwa timu ambazo zimepanda wakati huu pia zipo ambazo zinaweza kupanda kupitia play off nazo pia kazi yao iwe moja kupambana bila kuogopa. 


Imani yangu ni kwamba zile ambazo zimepanda zinatambua kwamba kuna ushindani mkubwa kwenye ligi na wanatambua pia lipo suala la kushuka.

Tunataka kuona timu ikipanda kwenye ligi iwe na uwezo na vigezo vya kuhimili mikikimikiki ya huku kwani hakuna kuzubaa ni mwendo wa kukimbizana.

Siri ya kufanya vizuri kwenye mechi za ligi ni maandalizi mazuri kwa wakati huu ni lazima kila mmoja awe tayari kwa ajili ya mechi zote ambazo atacheza kwa msimu ujao ambao nao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Jambo lingine ambalo wachezaji wanapaswa kutambua ni kwamba nidhamu ni suala la lazima kwao ikiwa wanahitaji kufikia mafanikio yao kila wakati.

Itawafanya waweze kuwa bora muda wote ndani ya uwanja na kuyafikia mafanikio yao pamoja na yale ya timu kiujumla kwa kuwa inawezekana kufanya hivyo.

Ninaona kwamba msimu ujao ushindani utakuwa mara dufu zaidi ya sasa kutokana na uwekezaji ambao umefanywa hivyo ni suala la kusubiri na kuona mambo yatakuwaje lakini jambo la muhimu ni kujipanga.

Kwa wale ambao wanaendelea na usajili niwakumbushe kwamba wakati unakuja na upo karibu. Kwa wachezaji wapya wana kazi ya kutambua kwamba wana kazi ya kufanya kwa ajili ya timu zao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here