Home Simba SC WAKATI LUIS AKIIBUKIA AL AHALY… MUGALU HUYOO APATA SHAVU TIMU KUTOKA MOROCCO

WAKATI LUIS AKIIBUKIA AL AHALY… MUGALU HUYOO APATA SHAVU TIMU KUTOKA MOROCCO


Kocha mkuu wa Klabu ya RS Berkane ya Morocco Florent Ibenge emeutaka uongozi wa klabu hiyo kutuma ofa kwa Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC, kumsajili mshambuliaji wa Simba SC Chris Mutshimba Kope Mugalu.

Mshambuliaji huyo raia wa DR Congo amekua na kiwango kizuri kwa msimu uliopita (2020/21), huku akimaliza nafasi ya pili katika orodha ya wapachika mabao, nyuma ya Bocco kwa kufunga mabao 15.

Ibenge ambaye alitimkia RS Berkane akitokea AS Vita Club mwezi Julai, anaamini usajili wa Mugalu mwenye umri wa miaka 30 kama utafanikiwa, atakua na safu kali ya ushambuliaji kwenye kikosi chake.

Hata hivyo Uongozi wa Simba SC, haujawahi kutangaza mpango wa kumuuza Mugalu katika kipindi hiki cha usajili wa kuelekea msimu 2021/22.

Simba SC ilimsajili Mugalu wakati wa usajili wa 2020/21 akitokea Power Dynamol ya Zambia.

SOMA NA HII  MAGORI AVUNJA UKIMYA SIMBA...AFUNGUKA A-Z TUHUMA ZA MO DEWJI..ATOA WITO HUU KWA MASHABIKI