Home Taifa Stars WALIOITWA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA WAFANYE KAZI, MAANDALIZI MUHIMU

WALIOITWA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA WAFANYE KAZI, MAANDALIZI MUHIMU


 KAMBI zinazidi kuendelea kwa sasa kwa timu shiriki katika Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza kwa sasa Championship Tanzania mpaka Ligi ya Wanawake Tanzania.

Baada ya ligi kumalizika na Simba kuwa mabingwa, timu sasa zinapata nafasi ya  kuongeza nguvu kwenye vikosi vyao.

 Ngoja nikukumbushe, Simba na Yanga zitawakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Azam FC pamoja na Biashara United zitacheza Kombe la Shirikisho.

Wote hawa wana kazi ya kufanya kuhakikisha kwamba wanafanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa ili kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa na inawezekana.

Ngoma bado inapigwa kwa timu kuzidi kujipanga ili kufanya vizuri. Katika hilo umakini unahitajika na kila mmoja ni muhimu kutimiza majukumu yake.

Kila kitu kwa sasa kinaendelea, naona pia zipo timu ambazo zimeanza kuzindua uzi mpya hilo ni jambo la msingi na jema kwa wakati huu kuendelea kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.

Pia wachezaji wengine kwa sasa wakiwa kwenye maandalizi wamechaguliwa kujiunga na timu ya taifa ya Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya kuwania tiketi ya kufunzu Kombe la Dunia.

Agosti 24 kambi iliweza kuanza kwa vijana waliochaguliwa kuanza kazi. Katika hilo ni muhimu kila mmoja kuweza kupambana katika kutimiza majukumu yake.

Iwe ni hatua njema kwa kila aliyeitwa kupambania jezi ya timu ya taifa. Hakuna namna ya kufanya kwa wakati mwingine kwa kuwa ukiitwa katika timu umeaminiwa.

Mashabiki wanahitaji kuona kwamba matokeo yanapatikana kwenye mechi zote. Hilo lipo wazi hata mashabiki nao wanajua kwamba kinachotakiwa kupatikana na ushindi hakuna jambo jingine.

Ile hali ya kuwa wasindikizaji kwenye mashindano ambayo tunashiriki kwa sasa naona muda wake umekwisha. Kinachotakiwa ni kwa kila mchezaji kufanya kazi kwa juhudi.

Pale kambi itakapoitwa basi zile chenga za hapa na pale zisiwepo. Nakumbuka kuna wakati fulani timu iliitwa kambini wachezaji wa Simba asilimia kubwa walipigwa chini kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utovu wa nidhamu.

Katika hilo kuna watu wengine walifungiwa masuala ya kushiriki kwenye ligi na kufanya uwepo wa makocha wengine. Hili hakileti picha nzuri.

SOMA NA HII  HIZI HAPA 'MASHINE NANE ZA KIMATAIFA' ZINAZOIPIGANIA HESHIMA YA BENDERA YA TANZANIA...

Kila la kheri wale ambao mmechaguliwa kuipeperusha bendera ya Tanzania. Mkiwa kambini fanyeni kazi mchana mpaka  kunapambazuka.

Yote kwa yote, mashabiki nao pia muhimu kufanya kazi kwa juhudi kutimiza majukuu ya taifa,kila la kheri.