Home Yanga SC YANGA KUANZA KUWAVUTIA KASI WANAIJERIA, KAMBI YAO MOROCCO KUANZA LEO

YANGA KUANZA KUWAVUTIA KASI WANAIJERIA, KAMBI YAO MOROCCO KUANZA LEO


 HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari ya Yanga amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya mechi za kimataifa yapo vizuri kwa kuwa wanahitaji kupata matokeo chanya.

Yanga katika mashindano ya kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika imepangwa na Wanaijereia kwenye hatua ya awali ambapo mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kati ya tarehe 10/12 wanaweza wakacheza mchezo huo Uwanja wa Mkapa na itacheza na Rivers United FC.

Msimu huu kwenye mashindano ya kimataifa itakuwa na wachezaji wake wapya ikiwa ni pamoja na Heritier Makambo, Fiston Mayele, Jesus Morocco.

Bumbuli amesema:-“Kambi tunaanza tarehe 15 tutakapokuwa tumefika Morocco kwa hiyo mpaka tarehe 26 kambi itakuwa imekamilika, tarehe 27 timu itarejea Dar es Salaam kwa wachezaji wote kwa ajili ya kushiriki tamasha la Wananchi kwenye kile kilele.

“Baada ya hapo kutakuwa na mapumziko kati ya tarehe nne na tano kutakuwa na mapumziko kwa wachezaji kwa ajili ya Kombe la Dunia, kuna wachezaji ambao wataitwa timu zao za taifa watakwenda kwenye mataifa yao.

“Tarehe 8, 6 watakuwa wanarejea kwa ajili ya kujiandaa na mtanage wa awali. Kwa hiyo tunaamini kwamba wale wachezaji wetu wengi kama wataitwa timu za taifa watakuwa huko na wale ambao watabaki baada ya kilele cha wiki ya Mwananchi wataendelea na maandalizi,” .

Chanzo:Azam TV


SOMA NA HII  KISA MECHI DHIDI YA AZAM...NABI APINGA MAAMUZI YA MABOSI WA YANGA...WASALIMU AMRI