Home Yanga SC YANGA WATAJA SABABU YA KUACHANA NA MAKIPA WAO WOTE WAWILI

YANGA WATAJA SABABU YA KUACHANA NA MAKIPA WAO WOTE WAWILI


 UONGOZI wa Yanga umeeleza kuwa sababu kubwa ya kuachana na nyota zao wawili ambao ni makipa ni kufuata ripoti ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Ni Metacha Mnata na Faroukh Shikalo ambao wote kandarasi zao zilikuwa zimemeguka na Nabi hakuwa tayari kuona wakiongezewa mkataba.

Kwa mujibu wa Haji Mfikirwa, Kaimu Katibu wa Yanga amesema kuwa ilikuwa ni mapendekezo ya kocha kuachana na wachezaji hao wote wawili.

“Tunafanya kazi kwa kuzingatia ripoti ya mwalimu hivyo ni yeye ambaye alipendekeza tufanye hivyo na hakuna namna nyingine.

“Mnata yeye amepewa barua leo ya kuwa mchezaji huru hivyo tunamtakia kila la kheri pamoja na Shikalo,” amesema.

SOMA NA HII  HII HAPA REKODI YA SIMBA NA YANGA...HAIJAVUNJWA KWA MIAKA 45...MSUVA NA SAMATTA WASALENDA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here