Home Cecafa Cup YANGA YATOSHANA NGUVU NA ATLABARA UWANJA WA MKAPA

YANGA YATOSHANA NGUVU NA ATLABARA UWANJA WA MKAPA


 KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha wa Makipa, Razack Siwa leo Agosti 4 kimelazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Klabu ya Atlabara.

Ni kwenye mchezo wa Kombe la Kagame ambao umechezwa Uwanjwa Mkapa na kushuhidiwa na baadhi ya mashabiki ambao walijitokeza pia wengine walishuhudia mubashara kupitia Azam Tv.

Dakika 90 zilikamilika kwa timu zote kutoshana nguvu na kugawana pointi mojamoja katika mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Nyota wao Wazir Junior ambaye ni mshambuliaji amesema kuwa bado wataendelea kupambana ili kupata matokeo kwenye mchezo wao ujao.

Ikumbukwe kwamba mchezo wao uliopita waligawana pointi mojamoja na Big Bullets kwenye mchezo wa ufunguzi ambapo Junior alifunga bao kwa Yanga kwa pasi ya Dickson Ambundo.

Matokeo ya leo yanaifanya Yanga kuwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi A na ina pointi 2 vinara ni Express wenye pointi nne ambao mchezo wao wa mwisho watakutana.

SOMA NA HII  KISA KUGOMBEA URAIS JANGWANI...SALEH JEMBE AMLIPUA INJINIA HERSI...ADAI KAZI YA UONGOZI YANGA HAINA MSHAHARA...