Home Uncategorized ARSENAL WATEMBEZA KICHAPO CARABAO CUP

ARSENAL WATEMBEZA KICHAPO CARABAO CUP

 


ARSENAL imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AFC Wimbledon katika mchezo wa Carabao Cup ikiwa ni hatua ya raundi ya tatu.


Ni mabao ya Alexander Lacazette dakika ya 11 kwa mkwaju wa penalti na bao la pili lilipachikwa dakika ya 77 na Emile Smith Rowe lile la pili lilipachikwa na Eddie Nketiah dakika ya 80.


Arsenal ikiwa Uwanja wa Emirates iliweza kupiga jumla ya mashuti 19 na ni matano yalilenga lango na wapinzani wao walipiga mashuti manne na hawakuwa na shuti hata moja ambalo lililenga lango.

Umiliki wa mpira ilikuwa ni asilimia 63 kwa Arsenal na 37 kwa wapinzani wao.

SOMA NA HII  YONDANI ALIPWA NUSU YA FEDHA ZAKE LAKINI ......

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here