Home news HUYU NDIYE DITRAM NCHIMBI HATARI YAKE KILA BAADA YA DAKIKA 243..ACHEZA MECHI...

HUYU NDIYE DITRAM NCHIMBI HATARI YAKE KILA BAADA YA DAKIKA 243..ACHEZA MECHI NNE TU


 NYOTA wa Yanga, Ditram Nchimbi aarufu kama Duma kwa msimu wa 2020/21 alikuwa na hatari ya kufunga ama kutengeneza nafasi ya bao kila baada ya dakika 243.

Ni bao moja alifunga ilikuwa Uwanja wa Mkapa akiwa nje ya 18 kwa mguu wake la kulia dakika ya 18 Aprili 20 mbele ya Gwambina FC ya Mwanza ambayo imeshuka daraja na msimu ujao itashiriki Championship Tanzania zamani ilikuwa inaitwa Ligi Daraja la Kwanza.

Pasi za mabao alitoa tatu ilikuwa mbele ya Biashara United akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kulia ilikuwa Uwanja wa Karume, Oktoba 31,2020.Pasi ya pili alitoa Uwanja wa Februari17, Uwanja wa Mkapa akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kulia mbele ya Kagera Sugar.

Pasi yake ya tatu kwa msimu wa 2020/21 ilikuwa mbele ya Dodoma Jiji kwa mguu wa kushoto Mei 19 mbele ya JKT Tanzania ambayo msimu ujao wa 2021/22 itashiriki Championship Tanzania, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Nchimbi alicheza jumla ya mechi 25 na ni mechi tano aliyeyusha dakika 90 huku mechi 20 akikwama kuyeyusha dakika zote 90.

Alizomaliza dakika 90 ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons, Simba,JKT Tanzania,Gwambina na Dodoma Jiji.

Ambazo hakuyeyusha dakika 90 mwendo wake ulikuwa namna hii:- dakika 21 mbele ya Mbeya City,dakika 2 mbele ya Mtibwa Sugar, dakika 31 mbele ya Polisi Tanzania, dakika 82 mbele ya Biashara United, dakika 8 mbele ya Gwambina, dakika 18 mbele ya Namungo, dakika 70 mbele ya Azam FC, dakika 5 mbele ya Ruvu Shooting, dakika 11 mbele ya Mwadui FC.

Dakika 1 mbele ya Dodoma Jiji,dakika 16 mbele ya Mbeya City,dakika 45 mbele ya Kagera Sugar, dakika 71 mbele ya Mtibwa Sugar, dakika 61 mbele ya Polisi Tanzania.

Dakika 14 mbele ya KMC,dakika 7 mbele ya Biashara United, dakika 32 mbele ya Azam FC, dk 28 mbele ya Namungo, dk 82 mbele ya JKT Tanzania, dk 27 mbele ya Simba.

SOMA NA HII  KWA BUKU 5 TU...UNAHAKIKA YA KUVUNA MPAKA MIL 3 ZA MERIDIANBET...ZINGATIA HAYA...

Jumla katika mechi 25 ambazo alicheza aliyeyusha dakika 973 akiwa amehusika katika mabao manne kati ya 52 ambayo yalifungwa na timu hiyo katika mechi 34 kwa kuwa alifunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.Ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 243.