Home KMC FC KMC WATIBULIWA MIPANGO YAO,NGOMA INAPIGWA KARATU

KMC WATIBULIWA MIPANGO YAO,NGOMA INAPIGWA KARATU


UONGOZI wa KMC, umeweka wazi kuwa suala la kubadilishiwa sehemu ya kucheza kwao limekuwa ni jambo linalowaumiza kwa kuwa ni mwanzo wa ligi jambo ambalo linahitaji kutazamwa kwa umakini.

Kesho KMC ina kazi ya kusaka ushindi mbelebya Polisi Tanzania katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Karatu, awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa Uwanja wa Ushirika, Moshi.

Kabla ya mchezo kuchezwa kesho umebadilishwa viwanja mara mbili ambapo ulipelekwa Sheikh Amri Abeid kisha ukapelekwa Karatu.

Christina Mwagala,  Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa kwa kilichotokea kimewavuruga hasa kutokana kuwa na strategic,  (mpango kazi) uliokuwa ukibadilika mara kwa mara.

Mwagala amesea:”Taarifa ya awali kwa mujibu wa Bodi ya Ligi Tanzania ilikuwa inaonyesha kwamba mchezo wetu utachezwa Uwanja wa Ushirika na hilo nilitoa taarifa awali kwamba tutacheza Uwanja wa Ushirika.

“Baadaye tukaambiwa kwamba mchezo utachezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kabla hatujafika huko tukaambiwa kwamba mchezo utakuwa Karatu.

“Haina maana kwamba hatuwezi kucheza hapana, sisi tunacheza popote lakini hii ni timu ina bajeti yake na kila mchezo kunapangwa strategic zake, awali tulipanga strategic za Ushirika kabla hatujazitumia ikabadilika na imebadilika tena.

“Katika hili muhimu ni kuona kwamba utaratibu unafuatwa na kutazama namna bora itakayofanya mambo yaende hasa ukizingatia ni mwanzo wa ligi,”.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPONA NA KUSHUKA DARAJA...MTIBWA SUGAR WAOMBA KUVUTA PUMZI ISHU YA USAJILI MPYA...