Home news KOCHA AZAM FC AKUBALI MUZIKI WA KANOUTE WA SIMBA

KOCHA AZAM FC AKUBALI MUZIKI WA KANOUTE WA SIMBA


 KWA sasa habari ya mjini ni kiungo mkabaji wa Simba, Sadio Kanoute, raia wa Mali, ambaye amefanikiwa kuonyesha kiwango bora kwenye mechi za maandalizi ya msimu ya timu hiyo, ishu hiyo imemuibua kocha wa zamani wa Azam, Ndanda na Lipuli, meja mstaafu Abdul Mingange ambaye amefunguka kuwa kiungo huyo atakuwa tishio msimu huu.

 

Kanoute alionyesha kiwango bora kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe uliopigwa Jumapili iliyopita licha ya Simba kupoteza kwa bao 1-0 lakini kiungo huyo alionyesha kiwango bora akipoteza pasi nne tu kati ya 39 alizopiga, akifanikiwa kutengeneza utulivu kwenye eneo la kiungo la Simba.

 

Akizungumza na Championi IjumaaMingange alifunguka: “Nimemuangalia huyu Kanoute ni mchezaji wa viwango vya juu, niwapongeze waliohusika kwenye usajili wake kwani ni mchezaji ambaye anatimiza majukumu yake ipasavyo hivyo.


“Namuona mmoja wa wachezaji ambao watafanya vizuri msimu huu, kwani amezoea mazingira kwa haraka tofauti na wachezaji wengine ambao huwa wanashindwa kuonyesha makali kwenye msimu wao wa kwanza wakiwa na timu mpya.”

 

Kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani zao Yanga utakaopigwa kesho Jumamosi, kwa Mkapa, Dar.

SOMA NA HII  TAKWIMU ZINAONGEA: SIMBA WAONGOZA MSIMAMO KWA KUKOSA PENATI...YANGA MHHH...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here