Home news KOCHA MPYA MTIBWA SUGAR MATUMAINI KIBAO

KOCHA MPYA MTIBWA SUGAR MATUMAINI KIBAO


 UONGOZI wa Klabu ya Mtibwa Sugar umempa mkataba wa miaka miwili kocha Joseph Omong kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho katika msimu mpya wa 2021/22.

Omog, mwenye uraia wa Cameroon, ametua kikosini hapo kwa ajili ya kuchukua mikoba ya kocha Mohammed Badru ambaye mkataba wake ulifika ukingoni.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru, alisema kuwa tayari wamempatia mkataba kocha huyo kwa ajili ya kukinoa kikosi chao huku wakiwa na matumaini ya kuwa mwalimu huyo atawafikisha katika malengo yao.

“Omog aliwasili hapa Jumatano na tumeshafanya makubaliano yote na kufikia maamuzi ya kumpa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kukinoa kikosi chetu na nipende kusema kuwa huyu ndio mwalimu wetu rasmi.

“Kupitia kocha huyu nina imani tutaweza kufikia malengo tuliyojiwekea sisi kama timu ambayo ni kuwa katika nafasi za juu za Ligi Kuu Bara kwa msimu huu,” alisema Kifaru.

Kwa upande wake Omog alifunguka: “Nina furaha kurejea tena Tanzania kwa mara nyingine, lakini kwa sasa nikiwa na kikosi cha Mtibwa matarajio yangu ni kufanya vizuri kama nilivyofanya kwenye timu nyingine huko nyuma, kwa usajili ambao umefanyika nina imani tutakwenda kufanya vizuri msimu huu.

“Uongozi umenihakikishia mazingira mazuri ya kazi hivyo ninatarajia makubwa kutoka kwa wachezaji wangu ambapo kupitia wao tutapambana kuiweka Mtibwa kwenye nafasi nzuri.”

SOMA NA HII  KAGERE, KIBU DENIS KUONGOZA MASHAMBULIZI DHIDI YA RUVU SHOOTING...KIKOSI KAMILI HIKI HAPA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here