Home news MANARA: WINGI WA MAKOMBE YA SIMBA NI WA MABONANZA

MANARA: WINGI WA MAKOMBE YA SIMBA NI WA MABONANZA


MSEMAJI wa Yanga, Haji Manara amefunguka kuwa wingi wa makombe ambayo alikuwa akiyazungumza akiwa Simba unajumuisha michuano ambayo ilikuwa ni ya mabonanza.

Agosti 24, mwaka huu kupitia mkutano na waandishi wa habari, Yanga ilimtambulisha rasmi Manara kuwa msemaji wao mpya, huku zikiwa zimepita siku chache tangu aachwe na Simba.

Tangu kuondoka kwake ndani ya Simba, Manara mara kwa mara amekuwa akizungumza kauli zenye tafsiri ya utata kuwahusu baadhi ya viongozi wa Simba, na klabu hiyo.

Akizungumza katika kituo kimoja cha redio kuhusu utumishi wake ndani ya Simba, Manara amesema: “Moja ya kazi kubwa ambayo niliifanya labda ni kuonesha ukubwa feki, hiyo dhambi niliitendea vibaya sana Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na nipo tayari kuhukumiwa hata gerezani kwa kufanya ulaghai wa ukubwa ambao haupo.

“Nazungumzia uhalisia, mimi siku zote sijawahi kuwa Simba, mimi nilikuwa Yanga.”

Kuhusu wingi wa makombe ya Simba

“Unajua sisi watu wengi ambao tupo kwenye mpira huwa hatuzungumzi uhalisia, lakini narudia tena unaposimamia takwimu basi Yanga ndiyo klabu yenye mataji mengi ya Ligi Kuu hapa nchini, lakini pia ndiyo klabu yenye makombe mengi zaidi hapa nchini.

“Kuna watu wengine wataanza kuuliza mbona ulivyokuwa Simba ulitoa takwimu tofauti, watu wanapaswa kutofautisha porojo na uhalisia, unajuaje kama labda nilizungumza nikiwa nimelewa, na huo ndio uhalisia kama utahusisha na takwimu za makombe ya mabonanza.”

SOMA NA HII  SIMBA KUFUNGA GOLI LA USAJILI DK ZA JIONI....KIFAA CHA MAZEMBE CHANGOJEA MAJIBU TU...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here