Home news MORRISON AFUNGUKA MAISHA YAKE AKIWA YANGA..AMTAJA NUGAZ..ATUPA DONGO KWA MANARA

MORRISON AFUNGUKA MAISHA YAKE AKIWA YANGA..AMTAJA NUGAZ..ATUPA DONGO KWA MANARA


Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Berbard Morrison, amejitoa muhanga kwa kumkumbusha namna ya maisha aliyekua Msemaji wa klabu huyo Haji Manara.

Morrison amejipa jukumu hilo baada ya kuona Haji Manara amekuwa sehemu ya watu wanaoisema vibaya Simba SC, baada ya kuondolewa kwenye nafasi yake mwishoni mwa mwezi Julai.

Kiungo huyo kutoka nchini Ghana amempa somo Manara kwa kuandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagarm.

Morrison ameandika: “Niliondoka Yanga wakati tukiwa hatuna maelewano na bado hatuelewani, sijawahi kusema chochote kibaya dhidi ya klabu, @caamil, @antonionugaz au mashabiki, unajua kwanini, ni kwa sababu walikuwa wakinilisha, kunipenda na kunihudumia vizuri mara nyingi hivyo siwezi kuwakosea heshima kwa sababu nina matatizo nao. Hiyo ni heshima na busara bro.”

“Kamwe using’ate mkono unaokulisha au uliokulisha kabla.”

Kuna msemo unasema “Busara ni kawaida lakini sio kwa watu wa kawaida”

“Ni ushauri kwako kaka mkubwa. Ukweli unauma lakini usiumie.”

SOMA NA HII  UNAWEZA KUIBUKA NA USHINDI HADI MARA1000 YA DAU LAKO NA MERIDIANBET......!