Home Azam FC MTAMBO WA MABAO AZAM FC WAREJEA

MTAMBO WA MABAO AZAM FC WAREJEA


 MSHAMULIAJI wa Azam FC, Prince Dube ambaye ni mtambo wa mabao amesharejea katika kikosi hicho akitokea nchini Afrika Kusini.

Dube ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, George Lwandamina hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Horseed FC hatua ya awali.

Msimu uliopita ndani ya Ligi Kuu Bara alitupia mabao 14 akiwa ni namba moja kwa Azam FC ila kukaa kwake nje ya uwanja kwa muda mrefu kuliyeyusha ndoto zake za kuwa mfungaji bora.

Katika mchezo huo Azam FC iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 jambo ambalo linawapa nafasi kubwa ya kusonga mbele licha ya kwamba bado kuna dakika 90 za maamuzi kwenye mchezo huo.

Alirejea Tanzania Jumatatu, Septemba 13 alfajiri akitokea kwenye matibabu jijini Cape Town, Afrika Kusini.

Dube amefanyiwa upasuaji mdogo, utakaomfanya akae nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita hivyo ataukosa pia mchezo wa marudio unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Septemba 18.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AITISHA KIKAO CHA DHARULA SIMBA KISA HIKI HAPA