Home news SIMBA YA MSIMU HUU WEKA MBALI NA WATOTO…ALLY MAYAY ASHINDWA KUJIZUIA..AFUNGUKA HAYA

SIMBA YA MSIMU HUU WEKA MBALI NA WATOTO…ALLY MAYAY ASHINDWA KUJIZUIA..AFUNGUKA HAYA

 


NI winga Peter Banda na Pape Ousmane Sakho unaoweza kukisia tayari wameingia moja kwa moja kikosi cha kwanza baada ya kuuzwa kwa Luis Miquissone na Clatous Chama.

Kutokana na maingizo mapya na uwepo wa nyota wao wa zamani Kocha Mkuu, Didier Gomes, atakuwa na kazi ngumu ya kufanya hasa safu ya ulinzi kuanzia kipa, beki wa kati na beki wa kulia kupata chaguo sahihi.

MANULA VS JEREMIAH KISUBI, KAKOLANYA

Simba wamebadilisha makipa mfululizo chini ya Manula. Amepita Deogratius Munishi ‘Dida’ na Said Mohamed ‘Nduda’, ila msimu huu picha limekuwa tofauti tangu walipomsajili Beno Kakolanya aliyekuwa na msimu mzuri akiwa na Yanga.

Sasa kuna Aishi Manula, Beno Kakolanya na Jeremiah Kisubi ni kazi kwa kocha Gomes kuamua nani aanze lakini vita kubwa ni kati ya Manula na Kisubi kwani Kakolanya ambaye ni kipa namba mbili tangu msimu uliopita hajaonyesha ushindani wa kutosha.

Kisubi ametua Simba akitokea Tanzania Prisons na alikuwa kipa namba moja kikosini humo akicheza michezo mingi na kuruhusu mabao machache makipa hao wawili wanaoingia vitani Manula amesave hatari 17 akiwa kipa aliyefanya majukumu makubwa zaidi msimu ulioisha wakati Kisubi 12.

HENOCK INONGA, JOASH ONYANGO VS PASCAL WAWA

Wawa ndiye beki mkongwe ndani ya safu hiyo akiiongoza Simba kutwaa mataji manne mfululizo anaingia vitani na Onyango ambaye pia tangu atue Simba amenyanyua kwapa mara mbili na Inonga ni msimu wake wa kwanza ndani ya kikosi hicho.

Inonga anapapangua ukuta wa Simba haswa katika eneo la beki ya kati ambao msimu huu wamekuwa wakicheza mara kwa mara, Pascal Wawa na Joash Onyango, Wawa au Onyango kuna mmoja atakwenda benchi ili kumpisha Mkongomani huyo kucheza kikosi cha kwanza kutokana na ubora wake aliouonyesha alikotoka .

Usimsahau Kennedy Juma. Anapiga jaramba nae kusaka namba katikati ya mastaa hao.

KAPOMBE VS ISRAEL PATRICK MWENDA

Patrick alikuwa panga pangua KMC sasa atampa changamoto mkongwe Kapombe ambaye sio kazi rahisi kumuondoa kikosi cha kwanza kutokana na ubora alionao. Kumbuka Simba iliachana usajili wa Djuma Shabaan aliyetua Yanga ili kumlinda Kapombe.

SOMA NA HII  KUELEKEA MSIMU UJAO....YANGA NI FULL KICHEKO...SIMBA WATAMBA KUTAWALA TENA CAF...

Ujio wa beki huyo si wa kwanza Simba kwani tayari alishapita David Kameta ‘Duchu’ aliyetolewa kwa mkopo Biashara Utd, huku Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na Gadiel Michael wataendeleza ligi yao upande wa kushoto.

WADAU WANENA

Nyota wa zamani Simba na Yanga, Zamoyoni Mogella alisema usajili waliofanya Simba ni mzuri kutokana na kuangalia zaidi maeneo ambayo yalikuwa na shida kwenye msimu uliopita.

Mogella alisema msimu uliopita Simba walionekana kuwa na shida hasa katika eneo la beki na sasa wamesajili hivyo wanasubiri kuona namna wachezaji wapya wataweza kuwa na utofauti gani.

“Mashabiki wana kawaida ya kusahau kama tu ukifanya vizuri, kikubwa kila nafasi wanayopata waitumie vizuri na watakubalika,” alisema Mogella, huku Ally Mayay alisema usajili wa Simba sio mkubwa sana kutokana na kusajiliwa wachezaji wachache kuongeza nguvu lakini wenye ubora mzuri na anaamini wataleta tija kikosini ligi ikianza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here