Home kimataifa WAKALI WA PASI ZA MWISHO HAWA HAPA

WAKALI WA PASI ZA MWISHO HAWA HAPA


 WAKATI timu zikiwa zinapambana kusaka ushindi kwa kutupia mabao mengi ndani ya uwanja kwenye ligi 5 pendwa duniani pia kuna vita nyingine ambayo inaendelea kwa wachezaji kupambana kuwa wapishi wa pasi za mwisho, ‘asisti’.

Hapa leo tunatazama wakali wa mipango ndani ya uwanja ambao kazi yao kubwa inakuwa kusoma upepo na kutoa pasi ndefu ama fupi itakayofika na mwisho wa siku kuweza kuleta bao kwa timu yake.

Kwa upande wa Ligi Kuu England ambayo moto umewaka kwa sasa kwa upande wa utengenezaji wa pasi za mwisho namba moja ni Paul Pogba kutoka Manchester United ni pasi 7 katengeneza jamaa huyu.

Timu yake kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza imekusanya pointi 10 baada ya kucheza mechi 4 na safu yao ya ushambuliaji imetupia mabao 11.

Ukija huku kwenye La Liga namba moja kwa pasi za mwisho ni Karim Benzema yeye yupo zake ndani ya Real Madrid na ametengeneza pasi nne za mabao. Timu yake ipo nafasi ya kwanza na pointi 10 baada ya kucheza mechi nne na imefunga jumla ya mabao 13,

Kwa upande wa Bundesliga ni Andrej Kramaric akiwa nazo nne na timu yake ya Honffenheim ipo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 4 baada ya kucheza mechi 4 imetupia maboa 8.

Seria A namba moja ni Nicolo Barella ambaye ametengeneza pasi tatu za mabao ndani ya timu ya Inter Milan ambayo ipo nafasi ya nne na pointi zake ni 7 safu yake ya ushambuliaji imetupia mabao 9. Pia yupo Luis Alberto anayekipiga Lazio ambayo ipo nafasi ya 7 ina pointi 6 huku safu yake ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 9.


Tukiangazia kwa upande wa Ligue 1 huko mkali wao ni Clauus na Frankowski hawa wote wawili wapo ndani ya Klabu ya Lens  wakiwa wametoa pasi tatutatu kila mmoja na timu yao ipo nafasi ya 5 na pointi zake ni 9 huku safu yao ya ushambuliaji imetupia mabao 10.

Pia mwingine ni Moses Simon ambaye ni mali ya Nantes ametupia pasi tatu timu yake ipo nafasi ya 14 ina pointi 4 na imetupia mabao matatu ambayo yote yeye ameyatengeneza.

SOMA NA HII  MANCHESTER CITY YAPELEKEWA MBELE SIKU YA KUTWAA TAJI LA LIGI KUU ENGLAND

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here