Home news YANGA WAPEWA MBINU YA KUPINDUA MEZA KIBABE LEO KIMATAIFA

YANGA WAPEWA MBINU YA KUPINDUA MEZA KIBABE LEO KIMATAIFA


 WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga wamepewa mbinu za kuweza kupindua meza kibabe nchini Nigeria na nyota wa zamani wa timu hiyo Mohamed Hussein, ‘Mmachinga’.

Leo Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi, ina kibarua kizito cha kusaka ushindi mbele ya Rivers United nchini Nigeria ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa kwa kufungwa bao 1-0.

Uzito wa mchezo wa leo upo katika ishu ya kupata ushindi wa mabao zaidi ya mawili na kuweza kuhakikisha kwamba ukuta wao hauruhusu bao ndani ya dakika 90 za machozi na jasho.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mmachinga alisema kuwa kwenye ulimwengu wa mpira kila kitu kinawezekana ikiwa wachezaji wa Yanga wataamua kufuata maelekezo ya benchi la ufundi na kucheza kwa kujiamini bila kukata tamaa.

“Kwa namna ulimwengu wa mpira ulivyo sasa kila kitu kinawezekana hata kupata matokeo ugenini inawezekana kwa kuwa wao waliweza kushinda kwetu basi kuna nafasi ya kwenda kushinda kwao pia.

“Kikubwa ambacho Yanga wanapaswa kufanya ni kuwa na nidhamu na kucheza kwa kufuata maelekezo ya benchi la ufundi, wachezaji wanajukumu la kufanya hivyo na inawezekana wakawapa furaha mashabiki na Tanzania kiujumla.

“Ni suala ambalo lipo kwenye uwezo wao na inawezekana. Mpira una njia na unahitaji nidhamu hivyo wawakilishi wetu bado wana nafasi ya kufanya vizuri” alisema Mmachinga. 

SOMA NA HII  SOKA LA BONGO LIMEENDELEA KUPASUA ANGA HUKO CAF UNAAMBIWA NAMBA HAZIDANGANYI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here