Home Yanga SC YANGA YAIPIGA BONGE MOJA YA MKWARA SIMBA, YALITAKA TAJI LA NGAO YA...

YANGA YAIPIGA BONGE MOJA YA MKWARA SIMBA, YALITAKA TAJI LA NGAO YA JAMII


 KUELEKEA kwenye Derby ya Simba na Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii, kocha wa Klabu ya Yanga, Nasreddine Nabi, amesema kuwa kikosi cha Yanga kimejiandaa vizuri kuelekea kwenye mchezo huo na hawezi kubashiri matokeo ya kesho licha ya kuwa amejiandaa kupata ushindi dhidi ya watani wao Simba Sc.

 

“Hii ni Derby ya tatu(3) tangu nijiunge na Yanga nina furaha kuwa sehemu ya benchi la ufundi la Yanga litakalo iongoza timu kupambana na Simba, mechi ya kesho sio tu derby ila ni fainali kwasababu ina kombe Uwanjani hivyo tumejiandaa vizuri na tumesahau habari za kuondoshwa kwenye klabu bingwa Afrika.

 

“Wachezaji na Benchi la ufundi tumejiandaa vizuri kwaajili ya mechi hiyo licha ya kuwa huwenda baadhi ya wachezaji hawana ‘match fitness’ ila wamejiandaa kupambana katika mchezo huo wa Ufunguzi wa Ligi.

 

“Kama kocha ‘Professional’ hawezi kuahidi matokeo ya aina yoyote ila kama kocha anafanya kazi na benchi la ufundi ili timu ipate ushindi hivyo katika Mechi ya kesho timu ni lazima kushinda kwasababu wamesha tolewa klabu bingwa Sasa wanaitaji kuwapa furaha mashabiki na viongozi kwa ujumla,” ameeleza Nabi.

 

Aidha Kocha Nabi ameongozea kuwa wachezaji Majeruhi ni Yasin Mustapha na Balama Mapinduzi na wameanza kufanya mazoezi mepesi japo hawataweza kuwa sehemu ya kikosi kitakacho chuana na Simba siku ya kesho.

 

“Wachezaji waliojiunga na timu wanaitaji kupambania namba ili kuingia kwenye kikosi kwa sababu wanahitaji kujuana na wenzao na kutengeneza muunganiko wa timu japo wapo watakaoanza moja kwa moja,” amesema Nabi.

SOMA NA HII  KOCHA ALIYEBORESHA KIWANGO CHA MANULA SIMBA ATUA YANGA KWA MBWEMBWE..ATOA KAULI HII....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here