Home news JEMBE LA KAZI SIMBA LAANZA MAZOEZI

JEMBE LA KAZI SIMBA LAANZA MAZOEZI


KIUNGO Sadio Kanoute nyota wa Simba amerejea mazoezini baada ya kuwa nje kwa muda akitibu majeraha aliyopata Septemba 25,2021 katika mchezo wa Ngao ya Jamii.


Katika mchezo huo ambao ulikuwa ni wa kwanza kwa ushindani kwa ingizo hilo jipya alikwama kuyeyusha dakika zote 90 baada ya kuumia katika harakati za kuipambania jezi ya Simba.
Mchezo huo ubao wa Uwanja wa Mkapa ulikamilika kwa kusoma Simba 0-1 Yanga na alishuhudia taji la kwanza kwa msimu wa 2021/22 likienda kwa watani zao wa jadi.
Kutokana na kuumia kwake amekosekana kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara ilikuwa ile ya ufunguzi mbele ya Biashara United na ile ya pili dhidi ya Dodoma Jiji.
Mchezo wa kwanza Simba iligawana pointi mojamoja na Biashara United baada ya kupata sare ya bila kufungana na ule mchezo wa pili Simba ilisepa na pointi tatu.
Ilikuwa mbele ya Dodoma Jiji baada ya ubao wa Uwanja wa Karume, Dodoma Jiji 0-1 Simba na mtupiaji alikuwa ni Meddie Kagere.
SOMA NA HII  PAMBANO LA IBRA CLASS NA MWALE WA ZAMBIA MAMBO NI MOTO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here