Home news KOCHA SIMBA ABAINISHA KWAMBA WANAKAMIWA

KOCHA SIMBA ABAINISHA KWAMBA WANAKAMIWA


 KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Didier Gomes amefunguka kuwa amebaini timu nyingi za ligi kuu huwa zinabadilika kiuchezaji zinapocheza dhidi yao na wachezaji huwa wanakamia sana.

Gomes amesema kwa sababu hiyo ameona jambo pekee ambalo wanatakiwa kwenda nalo ni kupata matokeo mapema ili kupunguza presha kwa wachezaji wakati mchezo ukiwa unaendelea.

Gomes amesema sababu kubwa ya wachezaji wake kufanyiwa madhambi mara kwa mara ni kutokana na wapinzani wao kucheza kwa kukamia na kulazimisha kupata matokeo mbele ya Simba.

 “Tumecheza mechi mbili za ligi na tumefanikiwa kuona nini tunatakiwa kufanya kwenye kila mchezo. Timu nyingi zikiwa zinacheza dhidi yetu huwa zinabadilika na kucheza kwa nguvu sana.

“Siyo jambo baya kwa sababu kila timu inahitaji matokeo, kwa upande wetu tumekaa chini na kujua nini tunatakiwa tufanye ili kuepukana na presha ndani ya uwanja, lazima dakika za mwanzo tuwe tumepata mabao,” amesema Gomes.

Mchezo wa ufunguzi wa ligi ilikuwa Uwanja wa Karume, Mara wale Wanajeshi wa Mpakani walionyesha maana halisi ya jina lao kwa kupambana na kugawana pointi mojamoja na mabingwa hao watetezi.

Ngoma ilikuwa Biashara United 0-0 Simba na nahodha John Bocco aliweza kukosa penalti dakika za jioni kwa mikono ya James Ssetupa kuokoa penalti hiyo.

Mchezo wa pili ilikuwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma hapo ubao ulisoma Dodoma Jiji 0-1 Simba na mtupiaji alikuwa ni Meddie Kagere dakika ya 69 kwa pasi ya Chris Mugalu.


SOMA NA HII  EDO KUMWEMBE AKOLEZA MOTO ISHU YA CHAMA KUMSIFIA MANARA INSTA, AMSHANGAA MO