Home news KUELEKEA MECHI DHIDI YA AZAM…AUCHO APEWA MAJUKUMU MAALUMU…KAZE AFUNGUKA…

KUELEKEA MECHI DHIDI YA AZAM…AUCHO APEWA MAJUKUMU MAALUMU…KAZE AFUNGUKA…

 


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, kweli anazitaka pointi tatu za Azam FC baada ya kuwataka viungo wake, Khalid Aucho na Yannick Bangala kupiga pasi nyingi za haraka kwenda katika goli la wapinzani.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Spoti Xtra, kwa niaba ya Kocha Nabi, Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze, alisema wao

benchi la ufundi wanataka kuona timu inacheza soka la kisasa la pasi nyingi kwa lengo la kuwapa burudani mashabiki wao.

Kaze alisema kuwa, anafurahia kuona timu yao ikiendelea kupata matokeo mazuri ya ushindi huku akiwazuia wachezaji wake kubutua mipira katika michezo yao.

Aliongeza kuwa, benchi lao la ufundi likiwa linaendelea kutengeneza muunganiko, wanataka kuona viungo Aucho, Bangala na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wakitimiza majukumu yao ya kuchezesha timu na kupiga pasi za uhakika za kuzaa mabao.

“Katika michezo ambayo tumecheza ya ligi, timu imeonekana ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga, pongezi nyingi ziende kwa viungo ambao wanatimiza vema majukumu yao.

“Kilichobakia hivi sasa ni kuona viungo wakituliza mashambulizi kwa kupiga pasi nyingi za haraka huku wakiendelea kushambulia goli la wapinzani katika michezo ijayo ukiwemo dhidi ya Azam.“

Mchezo wetu dhidi ya Azam siyo mdogo ni mkubwa kutokana na ubora wa timu yao, lakini kikubwa kama makocha tunataka kuona wachezaji wetu wanafanyia kazi mafunzo na maelekezo yetu tuliyokuwa tunaendelea kuwapa,” alisema Kaze.

SOMA NA HII  TRY AGAIN ATAMBA KUMSAJILI STRAIKA WA UHISAPANIA SIMBA HII SIO POA