Home news RASMI..ILI KUWAMALIZA WABOTSWANA MAPEMA…GOMES AMVIKA DUNCAN MAJUKUMU YA CHAMA NA LUIS

RASMI..ILI KUWAMALIZA WABOTSWANA MAPEMA…GOMES AMVIKA DUNCAN MAJUKUMU YA CHAMA NA LUIS


KATIKA kuhakikisha Jwaneng Galaxy ya Botswana inapasuka mapema Kwa Mkapa, Kocha Didier Gomes ameonekana akimpa kazi maalumu winga wake mpya Duncan Nyoni mazoezini na Mmalawi huyo hakumuangusha.

Duncan aliyesajiliwa hivi karibuni, alipewa kazi ya kupiga friikikii, huku timu nzima ikipewa mbinu za kukaba na kushambulia kwa pamoja kuonyesha kuwa leo Wabotswana watakuwa na kazi kubwa kwa Wekundu wa Msimbazi hao.

Soka la Bongo imefuatilia mazoezi ya Simba yanayoendelea Uwanja wa Boko Veterani, lilishuhudia baada ya programu za kukaba na kushambulia kumalizika, Gomes aliwaita Duncan, Bernard Morrison, Rally Bwalya, Erasto Nyoni, Israel Mwenda, Mohamed Hussein na Thadeo Lwanga na kuanza kuwapa somo namna ya kupiga frii kiki.

Walisogea katika moja ya goli la uwanja ule na kupanga midoli iliyosimikwa kama watu walioweka ukuta, langoni akiwepo Ally Salum kisha kuanza kupiga kwa kupokezana na aliyeshindwa mara nyingi alitoka na hatimaye kubaki Bwalya na Duncan.

Wawili hao walionyesha ubora zaidi huku Duncan akifunika kwa kufunga frii-kiki zile akitupia kambani zaidi ya mara tano na baada ya hapo  Gomes alimsifu Duncan katika kupiga frii-kiki.

“Ni mtaalamu sana, anajua ni upande gani atapiga na nguvu gani ataweka mguuni ili kufunga. Nadhani atatusaidia sana katika hili kama tutapata frii-kiki akiwa uwanjani,” alisema Gomes na kuongeza;

“Baada ya kuondoka kwa Chama (Clatous) na Luis (Miquissone) ambao mara nyingi walikuwa wakipiga frii-kiki nadhani sasa atakuwa anapiga Duncan na kina Bwalya, Israel na Morrison.”

SOMA NA HII  SHAFFIH DAUDA AZIDI KUTIA 'KUTIA NDIMU' SAKATA LA SIMBA KUKATAA KUVAA NEMBO YA GSM..ADAI NI MSIBA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here