Home news STARS KAMILI KUIVAA BENIN KESHO KWA MKAPA

STARS KAMILI KUIVAA BENIN KESHO KWA MKAPA


MENEJA wa timu ya taifa ya Tanzania,  Taifa Stars, Nadir Haroub,’Cannavaro’ amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Benin.

Kesho Oktoba 7 Stars itakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia.

Canavaro amesema maandalizi na kila kitu kipo sawa hivyo ni suala la kusubiri muda wa mchezo utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.

“Kila kitu kipo sawa kwa kuwa tutakuwa nyumbani basi tutapambana ili kupata matokeo na tunaamini kwamba ushindani hautakuwa mdogo kwani timu zote zinahitaji matokeo,”.

Ni Jonas Mkude, Bakari Mwamnyeto,  Shomari Kapombe na Erasto Nyoni hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Stars kutokana na matatizo mbalimbali.

Mkude ana matatizo ya kifamilia huku Kapombe, Nyoni na Mwamnyeto hawa bado hawajawa fiti.

SOMA NA HII  SAKATA LA NTIBAZONKIZA NA AMBUNDO KUSIMAMISHWA...MANARA ASHINDWA KUJIZUIA...NAYE KAIBUKA NA HILI...